2 Wafalme 15:20
2 Kings 15:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Menahemu akatoza fedha hizi kwa nguvu kutoka kwa Israeli. Kila mtu tajiri alilazimika kuchanga shekeli hamsini za fedha* ambazo alipewa mfalme wa Ashuru. Basi mfalme wa Ashuru akajiondoa na hakuendelea kuikalia nchi.
2 Kings 15:20 in English
2 Kings 15:20 · Berean Standard Bible
Menahem exacted this money from each of the wealthy men of Israel—fifty shekels of silver * from each man—to give to the king of Assyria. So the king of Assyria withdrew and did not remain in the land.
Context
18Akatenda maovu machoni pa Bwana. Katika wakati wa utawala wake wote, hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati ambazo alisababisha Israeli kuzitenda. 19Kisha Pulu mfalme wa Ashuru akaishambulia Israeli. Menahemu mfalme wa Israeli akampa talanta elfu moja za fedha* ili amsaidie na kumwezesha katika utawala wake. 20Menahemu akatoza fedha hizi kwa nguvu kutoka kwa Israeli. Kila mtu tajiri alilazimika kuchanga shekeli hamsini za fedha* ambazo alipewa mfalme wa Ashuru. Basi mfalme wa Ashuru akajiondoa na hakuendelea kuikalia nchi. 21Matukio mengine ya utawala wa Menahemu na yote aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli? 22Menahemu akalala pamoja na baba zake. Naye Pekahia mwanawe akawa mfalme baada yake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.