2 Wafalme 10:26
2 Kings 10:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wakaileta ile nguzo ya kuabudiwa nje ya hekalu la Baali, na wakaichoma moto.
2 Kings 10:26 in English
2 Kings 10:26 · Berean Standard Bible
They brought out the sacred pillar of the temple of Baal and burned it.
Context
24Kwa hiyo wakaingia ndani ili kutoa kafara na sadaka ya kuteketezwa. Wakati huu, Yehu alikuwa amewaweka watu wake themanini akiwa amewapa onyo kwamba, “Ikiwa mmoja wenu atamwachia mtu yeyote ninayemweka mikononi mwake atoroke, itakuwa uhai wako kwa uhai wake.” 25Mara baada ya Yehu kutoa sadaka ya kuteketezwa, akawaamuru walinzi na maafisa: “Ingieni ndani, waueni; asitoroke hata mmoja.” Basi wakawakatakata kwa upanga. Walinzi na maafisa wakazitupa zile maiti nje, kisha wakaingia mahali pa ndani pa kuabudia miungu katika hekalu la Baali. 26Wakaileta ile nguzo ya kuabudiwa nje ya hekalu la Baali, na wakaichoma moto. 27Wakabomoa ile nguzo ya kuabudiwa ya Baali pamoja na hekalu la Baali, nao watu wakapafanya kuwa choo hadi leo. 28Kwa hiyo Yehu akaangamiza kuabudiwa kwa Baali katika Israeli.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.