2 Wakorintho 7:6
2 Corinthians 7:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Bali Mungu, yeye awafarijie wenye huzuni, alitufariji kwa kufika kwake Tito.
2 Corinthians 7:6 in English
2 Corinthians 7:6 · Berean Standard Bible
But God, who comforts the downcast, comforted us by the arrival of Titus,
Context
4Mara nyingi najivuna kwa ajili yenu; naona fahari juu yenu. Nimejawa na faraja. Nina furaha kupita kiasi katika mateso yetu yote. 5Kwa maana hata tulipoingia Makedonia, miili yetu haikuwa na raha. Tulisumbuliwa kila upande, kwa nje kulikuwa na mapigano na mioyoni mwetu tulikuwa na hofu. 6Bali Mungu, yeye awafarijie wenye huzuni, alitufariji kwa kufika kwake Tito. 7Lakini si kule kuja kwa Tito tu, bali pia kwa faraja mliyompa. Alitueleza jinsi mlivyonionea shauku, huzuni yenu kubwa na juhudi yenu kwa ajili yangu, ili kwamba furaha yangu ipate kuwa kubwa kuliko wakati wowote. 8Hata kama niliwahuzunisha kwa barua yangu, sijutii. Ingawa nilijuta kwa muda mfupi, kwa kuwa najua kwamba barua yangu iliwaumiza, lakini ni kwa kitambo tu,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.