Native Bible

2 Corinthians 6:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hatuweki kitu cha kukwaza katika njia ya mtu yeyote, ili huduma yetu isionekane kuwa na lawama.

2 Corinthians 6:3 in English

2 Corinthians 6:3 · Berean Standard Bible

We put no obstacle in anyone’s way, so that no one can discredit our ministry.

Context

1Kama watendakazi pamoja na Mungu, tunawasihi msipokee neema ya Mungu bure. 2Kwa maana asema: “Wakati wangu uliokubalika nilikusikia, siku ya wokovu nilikusaidia.” Tazama, wakati uliokubalika ndio huu, siku ya wokovu ndiyo sasa. 3Hatuweki kitu cha kukwaza katika njia ya mtu yeyote, ili huduma yetu isionekane kuwa na lawama. 4Bali kama watumishi wa Mungu tuonyeshe kwa kila njia: katika saburi nyingi; katika dhiki, katika misiba, na katika shida; 5katika kupigwa, katika kufungwa gerezani na katika ghasia; katika kazi ngumu, katika kukesha na katika kufunga;

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.