2 Wakorintho 3:4
2 Corinthians 3:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hili ndilo tumaini tulilo nalo mbele za Mungu kwa njia ya Kristo.
2 Corinthians 3:4 in English
2 Corinthians 3:4 · Berean Standard Bible
Such confidence before God is ours through Christ.
Context
2Ninyi wenyewe ndio barua yetu iliyoandikwa katika mioyo yetu, inayojulikana na kusomwa na kila mtu. 3Nanyi mwadhihirisha wazi kwamba ninyi ni barua itokayo kwa Kristo, matokeo ya huduma yetu, ambayo haikuandikwa kwa wino bali kwa Roho wa Mungu aliye hai, si katika vibao vya mawe, bali katika vibao ambavyo ni mioyo ya wanadamu. 4Hili ndilo tumaini tulilo nalo mbele za Mungu kwa njia ya Kristo. 5Si kwamba sisi tunafikiri kuwa tunaweza kufanya jambo lolote wenyewe, lakini nguvu yetu inatoka kwa Mungu. 6Ndiye alituwezesha sisi kuwa wahudumu wa Agano Jipya: si wa andiko, bali wa Roho; kwa kuwa andiko huua bali Roho hutia uzima.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.