Native Bible

2 Chronicles 5:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wazee wote wa Israeli walipofika, Walawi wakajitwika Sanduku la Agano,

2 Chronicles 5:4 in English

2 Chronicles 5:4 · Berean Standard Bible

When all the elders of Israel had arrived, the Levites took up the ark,

Context

2Kisha Solomoni akawaita huko Yerusalemu wazee wa Israeli, viongozi wote wa makabila na wakuu wa jamaa za Waisraeli, ili walilete Sanduku la Agano la Bwana kutoka Sayuni, Mji wa Daudi. 3Nao wanaume wote wa Israeli wakakusanyika kwa mfalme wakati wa sikukuu mwezi wa saba. 4Wazee wote wa Israeli walipofika, Walawi wakajitwika Sanduku la Agano, 5nao wakalipandisha Sanduku na Hema la Kukutania pamoja na vyombo vyote vitakatifu vilivyokuwa ndani yake. Makuhani, waliokuwa Walawi, walivibeba vitu hivyo, 6naye Mfalme Solomoni na kusanyiko lote la Israeli waliokusanyika kumzunguka walikuwa mbele ya hilo Sanduku, nao wakatoa dhabihu nyingi za kondoo na ngʼombe ambao idadi yao haikuwezekana kuandikwa au kuhesabiwa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.