2 Nyakati 4:11
2 Chronicles 4:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Pia akatengeneza masufuria, masepetu na mabakuli ya kunyunyizia. Kwa hiyo Huramu akakamilisha kazi katika Hekalu la Mungu kama vile Mfalme Solomoni alikuwa amemwagiza, yaani:
2 Chronicles 4:11 in English
2 Chronicles 4:11 · Berean Standard Bible
Additionally, Huram made the pots, shovels, and sprinkling bowls. So Huram finished the work that he had undertaken for King Solomon in the house of God:
Context
9Akatengeneza ukumbi wa makuhani na ukumbi mwingine mkubwa na milango yake, naye akaifunika hiyo milango kwa shaba. 10Akaweka ile Bahari upande wa kusini, kwenye pembe ya kusini mashariki ya nyumba. 11Pia akatengeneza masufuria, masepetu na mabakuli ya kunyunyizia.
Kwa hiyo Huramu akakamilisha kazi katika Hekalu la Mungu kama vile Mfalme Solomoni alikuwa amemwagiza, yaani: 12zile nguzo mbili;
yale mataji mawili yaliyokuwa juu ya hizo nguzo,
zile nyavu mbili za kupamba hayo mataji mawili yenye umbo la bakuli yaliyowekwa juu ya zile nguzo; 13yale makomamanga 400 kwa ajili ya hizo nyavu mbili (safu mbili za makomamanga kwa kila wavu yakipamba hayo mataji mawili yenye umbo la bakuli juu ya hizo nguzo);
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.