Native Bible

2 Chronicles 4:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Akaweka ile Bahari upande wa kusini, kwenye pembe ya kusini mashariki ya nyumba.

2 Chronicles 4:10 in English

2 Chronicles 4:10 · Berean Standard Bible

He put the Sea on the south side, at the southeast corner.

Context

8Akatengeneza meza kumi na kuziweka hekaluni, tano upande wa kusini na tano upande wa kaskazini. Pia akatengeneza mabakuli 100 ya dhahabu ya kunyunyizia. 9Akatengeneza ukumbi wa makuhani na ukumbi mwingine mkubwa na milango yake, naye akaifunika hiyo milango kwa shaba. 10Akaweka ile Bahari upande wa kusini, kwenye pembe ya kusini mashariki ya nyumba. 11Pia akatengeneza masufuria, masepetu na mabakuli ya kunyunyizia. Kwa hiyo Huramu akakamilisha kazi katika Hekalu la Mungu kama vile Mfalme Solomoni alikuwa amemwagiza, yaani: 12zile nguzo mbili; yale mataji mawili yaliyokuwa juu ya hizo nguzo, zile nyavu mbili za kupamba hayo mataji mawili yenye umbo la bakuli yaliyowekwa juu ya zile nguzo;

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.