2 Nyakati 27:2
2 Chronicles 27:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Akafanya yaliyo mema machoni pa Bwana kama Uzia baba yake alivyokuwa amefanya, lakini tofauti na yeye, hakuingilia huduma za hekaluni mwa Bwana. Lakini hata hivyo, watu wakaendelea na desturi zao mbaya.
2 Chronicles 27:2 in English
2 Chronicles 27:2 · Berean Standard Bible
And he did what was right in the eyes of the LORD, just as his father Uzziah * had done. In addition, he did not enter the temple of the LORD. But the people still behaved corruptly.
Context
1Yothamu alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka kumi na sita. Mama yake aliitwa Yerusha binti Sadoki. 2Akafanya yaliyo mema machoni pa Bwana kama Uzia baba yake alivyokuwa amefanya, lakini tofauti na yeye, hakuingilia huduma za hekaluni mwa Bwana. Lakini hata hivyo, watu wakaendelea na desturi zao mbaya. 3Yothamu akajenga upya Lango la Juu la Hekalu la Bwana na kufanya kazi kubwa kwenye ukuta katika kilima cha Ofeli. 4Akajenga miji katika vilima vya Yuda pamoja na ngome na minara mwituni.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.