Native Bible

2 Chronicles 20:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Watu fulani wakaja wakamwambia Yehoshafati, “Jeshi kubwa linakuja dhidi yako kutoka Edomu tokea ngʼambo ile nyingine ya Bahari.* Tayari liko Hasason-Tamari” (yaani En-Gedi).

2 Chronicles 20:2 in English

2 Chronicles 20:2 · Berean Standard Bible

Then some men came and told Jehoshaphat, “A vast army is coming against you from Edom,* from beyond the Sea;* they are already in Hazazon-tamar” (that is, En-gedi).

Context

1Ikawa baada ya jambo hili, Wamoabu na Waamoni, pamoja na baadhi ya Wameuni wakaja ili wapigane vita na Yehoshafati. 2Watu fulani wakaja wakamwambia Yehoshafati, “Jeshi kubwa linakuja dhidi yako kutoka Edomu tokea ngʼambo ile nyingine ya Bahari.* Tayari liko Hasason-Tamari” (yaani En-Gedi). 3Yehoshafati akaogopa, akaazimu kumtafuta Bwana, na akatangaza kwa Yuda wote kufunga. 4Watu wa Yuda wakakusanyika pamoja ili kutafuta msaada kutoka kwa Bwana. Wakaja kutoka kila mji wa Yuda ili kumtafuta.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.