Native Bible

2 Chronicles 14:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Akawaamuru Yuda kumtafuta Bwana, Mungu wa baba zao na kutii sheria zake na amri zake.

2 Chronicles 14:4 in English

2 Chronicles 14:4 · Berean Standard Bible

He commanded the people of Judah to seek the LORD, the God of their fathers, and to observe the law and the commandments.

Context

2Asa akatenda yaliyo mema na haki machoni pa Bwana Mungu wake. 3Akaziondoa madhabahu za kigeni na mahali pa juu pa kuabudia miungu, akayavunja yale mawe ya kuabudiwa na kuzikatakata nguzo za Maashera. 4Akawaamuru Yuda kumtafuta Bwana, Mungu wa baba zao na kutii sheria zake na amri zake. 5Akaondoa mahali pa juu pa kuabudia miungu na madhabahu za kufukizia uvumba kwenye kila mji katika Yuda, nao ufalme ulikuwa na amani katika utawala wake. 6Akajenga miji yenye ngome katika Yuda, wakati nchi ikiwa na amani. Hakuna mtu yeyote aliyepigana vita naye katika miaka hiyo, kwa kuwa Bwana alimstarehesha.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.