Native Bible

2 Chronicles 11:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Lakini neno hili la Bwana likamjia Shemaya mtu wa Mungu:

2 Chronicles 11:2 in English

2 Chronicles 11:2 · Berean Standard Bible

But the word of the LORD came to Shemaiah the man of God:

Context

1Ikawa Rehoboamu alipofika Yerusalemu, akakusanya nyumba ya Yuda na ya Benyamini, wanaume wapiganaji 180,000, kufanya vita dhidi ya nyumba ya Israeli na kuurudisha tena ufalme kwa Rehoboamu mwana wa Solomoni. 2Lakini neno hili la Bwana likamjia Shemaya mtu wa Mungu: 3“Mwambie Rehoboamu mwana wa Solomoni mfalme wa Yuda, na Israeli wote walioko Yuda na Benyamini, 4‘Hili ndilo asemalo Bwana: Msipande kupigana dhidi ya ndugu zenu. Nendeni nyumbani, kila mmoja wenu, kwa kuwa hili nimelitenda mimi.’ ” Kwa hiyo wakalitii neno la Bwana na wakaacha kwenda kupigana dhidi ya Yeroboamu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.