2 Nyakati 11:19
2 Chronicles 11:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mahalati alimzalia Rehoboamu wana: Yeushi, Shemaria na Zahamu.
2 Chronicles 11:19 in English
2 Chronicles 11:19 · Berean Standard Bible
She bore sons to him: Jeush, Shemariah, and Zaham.
Context
17Wakaimarisha ufalme wa Yuda na kumuunga mkono Rehoboamu mwana wa Solomoni miaka mitatu, wakienenda katika njia za Daudi na Solomoni katika wakati huu. 18Rehoboamu alimwoa Mahalati ambaye alikuwa binti Yeremothi mwana wa Daudi, mamaye alikuwa Abihaili binti Eliabu mwana wa Yese. 19Mahalati alimzalia Rehoboamu wana: Yeushi, Shemaria na Zahamu. 20Kisha akamwoa Maaka binti Absalomu, ambaye alimzalia: Abiya, Atai, Ziza na Shelomithi. 21Rehoboamu akampenda Maaka binti Absalomu zaidi kuliko wakeze wengine na masuria wake. Kwa jumla alikuwa na wake kumi na wanane na masuria sitini, wana ishirini na wanane na binti sitini.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.