2 Nyakati 10:18
2 Chronicles 10:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mfalme Rehoboamu akamtuma Adoniramu* aliyekuwa msimamizi wa wale waliofanya kazi ngumu kwa kulazimishwa, lakini Israeli wote wakampiga kwa mawe hadi akafa. Hata hivyo, Mfalme Rehoboamu, akafanikiwa kuingia kwenye gari lake na kutorokea Yerusalemu.
2 Chronicles 10:18 in English
2 Chronicles 10:18 · Berean Standard Bible
Then King Rehoboam sent out Hadoram,* who was in charge of the forced labor, but the Israelites stoned him to death. And King Rehoboam mounted his chariot in haste and escaped to Jerusalem.
Context
16Israeli wote walipoona kuwa mfalme amekataa kuwasikiliza, wakamjibu mfalme:
“Tuna fungu gani kwa Daudi?
Sisi hatuna urithi kwa mwana wa Yese.
Nendeni kwenye mahema yenu, ee Israeli,
angalia nyumba yako mwenyewe, ee Daudi!”
Hivyo Waisraeli wakaenda kwenye mahema yao. 17Lakini kwa habari ya Waisraeli waliokuwa wakiishi katika miji ya Yuda, Rehoboamu akaendelea kuwatawala bado. 18Mfalme Rehoboamu akamtuma Adoniramu* aliyekuwa msimamizi wa wale waliofanya kazi ngumu kwa kulazimishwa, lakini Israeli wote wakampiga kwa mawe hadi akafa. Hata hivyo, Mfalme Rehoboamu, akafanikiwa kuingia kwenye gari lake na kutorokea Yerusalemu. 19Hivyo Israeli wakaasi dhidi ya nyumba ya Daudi hadi leo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.