2 Nyakati 1:7
2 Chronicles 1:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Usiku ule Mungu akamtokea Solomoni na kumwambia, “Omba lolote utakalo nikupe.”
2 Chronicles 1:7 in English
2 Chronicles 1:7 · Berean Standard Bible
That night God appeared to Solomon and said, “Ask, and I will give it to you!”
Context
5Lakini yale madhabahu ya shaba ambayo Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, alikuwa ametengeneza yalikuwa huko Gibeoni mbele ya Maskani ya Bwana Mungu, hivyo Solomoni na kusanyiko lote walimtafuta Mungu huko. 6Solomoni akapanda huko yalikokuwa madhabahu ya shaba mbele za Bwana katika Hema la Kukutania, na kutoa dhabihu 1,000 za sadaka za kuteketezwa juu yake. 7Usiku ule Mungu akamtokea Solomoni na kumwambia, “Omba lolote utakalo nikupe.” 8Solomoni akamjibu Mungu, “Umemwonyesha baba yangu Daudi fadhili nyingi, nawe umeniweka niwe mfalme mahali pake. 9Sasa, Bwana Mungu, ahadi yako kwa baba yangu Daudi na ithibitike, kwa kuwa umenifanya mimi mfalme juu ya watu ambao ni wengi kama mavumbi ya nchi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.