1 Timotheo 5:3
1 Timothy 5:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Waheshimu wanawake wajane ambao ni wajane kweli kweli.
1 Timothy 5:3 in English
1 Timothy 5:3 · Berean Standard Bible
Honor the widows who are truly widows.
Context
1Usimkemee mzee kwa ukali bali umshawishi kama vile angekuwa ni baba yako. Uwatendee vijana kama vile ndugu zako; 2nao wanawake wazee uwatendee kama mama zako, na wanawake vijana kama dada zako, katika usafi wote. 3Waheshimu wanawake wajane ambao ni wajane kweli kweli. 4Kama mjane ana watoto ama wajukuu, hawa inawapasa awali ya yote wajifunze kutimiza wajibu wao wa kumcha Mungu katika matendo kwa kuwatunza wale wa jamaa zao wenyewe, na hivyo wawarudishie wema waliowatendea wazazi wao, kwa kuwa hivi ndivyo impendezavyo Mungu. 5Mwanamke ambaye ni mjane kweli kweli, yaani, yeye aliyebaki peke yake huweka tumaini lake kwa Mungu naye hudumu katika maombi usiku na mchana akimwomba Mungu ili amsaidie.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.