1 Timotheo 5:2
1 Timothy 5:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
nao wanawake wazee uwatendee kama mama zako, na wanawake vijana kama dada zako, katika usafi wote.
1 Timothy 5:2 in English
1 Timothy 5:2 · Berean Standard Bible
older women as mothers, and younger women as sisters, with absolute purity.
Context
1Usimkemee mzee kwa ukali bali umshawishi kama vile angekuwa ni baba yako. Uwatendee vijana kama vile ndugu zako; 2nao wanawake wazee uwatendee kama mama zako, na wanawake vijana kama dada zako, katika usafi wote. 3Waheshimu wanawake wajane ambao ni wajane kweli kweli. 4Kama mjane ana watoto ama wajukuu, hawa inawapasa awali ya yote wajifunze kutimiza wajibu wao wa kumcha Mungu katika matendo kwa kuwatunza wale wa jamaa zao wenyewe, na hivyo wawarudishie wema waliowatendea wazazi wao, kwa kuwa hivi ndivyo impendezavyo Mungu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.