1 Timotheo 5:14
1 Timothy 5:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hivyo nawashauri wajane vijana waolewe, wazae watoto na wasimamie nyumba zao, wasije wakampa adui nafasi ya kutushutumu.
1 Timothy 5:14 in English
1 Timothy 5:14 · Berean Standard Bible
So I advise the younger widows to marry, have children, and manage their households, denying the adversary occasion for slander.
Context
12Nao kwa njia hiyo watajiletea hukumu kwa kukiuka ahadi yao ya kwanza. 13Zaidi ya hayo, wajane kama hao huwa na tabia ya uvivu wakizurura nyumba kwa nyumba, wala hawawi wavivu tu, bali pia huwa wasengenyaji, wajiingizao katika mambo yasiyowahusu na kusema mambo yasiyowapasa kusema. 14Hivyo nawashauri wajane vijana waolewe, wazae watoto na wasimamie nyumba zao, wasije wakampa adui nafasi ya kutushutumu. 15Kwa maana kwa kweli wajane wengine wamepotoka ili kumfuata Shetani. 16Lakini kama mwanamke yeyote aaminiye ana wajane katika jamaa yake, inampasa awasaidie wala si kuwaacha wakililemea kanisa, ili kanisa liweze kuwasaidia wale ambao ni wajane kweli kweli.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.