Native Bible

1 Timothy 5:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Nao kwa njia hiyo watajiletea hukumu kwa kukiuka ahadi yao ya kwanza.

1 Timothy 5:12 in English

1 Timothy 5:12 · Berean Standard Bible

and thus will incur judgment because they are setting aside their first faith.

Context

10awe ameshuhudiwa kwa matendo yake mema, aliyewalea watoto wake vizuri, aliye mkarimu, aliyewanawisha watakatifu miguu, aliyewasaidia wenye shida na aliyejitolea kwa ajili ya matendo mema ya kila namna. 11Lakini kwa habari za wajane vijana usiwaweke kwenye orodha hiyo, maana tamaa zao za kimaumbile zikizidi kule kujitoa kwao kwa Kristo, watataka kuolewa tena. 12Nao kwa njia hiyo watajiletea hukumu kwa kukiuka ahadi yao ya kwanza. 13Zaidi ya hayo, wajane kama hao huwa na tabia ya uvivu wakizurura nyumba kwa nyumba, wala hawawi wavivu tu, bali pia huwa wasengenyaji, wajiingizao katika mambo yasiyowahusu na kusema mambo yasiyowapasa kusema. 14Hivyo nawashauri wajane vijana waolewe, wazae watoto na wasimamie nyumba zao, wasije wakampa adui nafasi ya kutushutumu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.