1 Timotheo 4:13
1 Timothy 4:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Fanya bidii kusoma Maandiko hadharani, kuhubiri na kufundisha, mpaka nitakapokuja.
1 Timothy 4:13 in English
1 Timothy 4:13 · Berean Standard Bible
Until I come, devote yourself to the public reading of Scripture, to exhortation, and to teaching.
Context
11Mambo haya yaagize na kuyafundisha. 12Mtu yeyote asikudharau kwa kuwa wewe ni kijana, bali uwe kielelezo kizuri kwa waumini katika usemi, mwenendo, upendo, imani na usafi. 13Fanya bidii kusoma Maandiko hadharani, kuhubiri na kufundisha, mpaka nitakapokuja. 14Usiache kutumia kipawa kilicho ndani yako, ambacho ulipewa kwa neno la unabii wakati wazee walikuwekea mikono. 15Uwe na bidii katika mambo haya; ujitolee kwa ajili ya mambo haya kikamilifu, ili kila mtu aone kuendelea kwako.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.