1 Timotheo 3:11
1 Timothy 3:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Vivyo hivyo, wake zao wawe wanawake wanaostahili heshima, wasio wasingiziaji, bali wawe na kiasi na waaminifu katika kila jambo.
1 Timothy 3:11 in English
1 Timothy 3:11 · Berean Standard Bible
In the same way, the women * must be dignified, not slanderers, but temperate and faithful in all things.
Context
9Inawapasa kushikamana sana na ile siri ya imani kwa dhamiri safi. 10Ni lazima wapimwe kwanza; kisha kama hakuna neno dhidi yao, basi na waruhusiwe kuhudumu kama mashemasi. 11Vivyo hivyo, wake zao wawe wanawake wanaostahili heshima, wasio wasingiziaji, bali wawe na kiasi na waaminifu katika kila jambo. 12Shemasi awe mume wa mke mmoja na inampasa aweze kusimamia watoto wake na watu wa nyumbani mwake vyema. 13Wale ambao wamehudumu vyema katika huduma ya ushemasi hujipatia msimamo bora na ujasiri mkubwa katika imani yao ndani ya Kristo Yesu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.