Native Bible

1 Timothy 1:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kusudi la maagizo haya ni upendo utokao katika moyo safi, dhamiri njema na imani ya kweli.

1 Timothy 1:5 in English

1 Timothy 1:5 · Berean Standard Bible

The goal of our instruction is the love that comes from a pure heart, a clear conscience, and a sincere faith.

Context

3Kama nilivyokusihi wakati nilipokwenda Makedonia, endelea kubaki Efeso, ili kwamba upate kuwaagiza watu wasiendelee kufundisha mafundisho ya uongo 4wala wasitoe muda wao kwa hadithi za kubuniwa na orodha za majina ya vizazi visivyo na mwisho, ambazo huchochea mabishano badala ya mpango wa Mungu utokanao na imani. 5Kusudi la maagizo haya ni upendo utokao katika moyo safi, dhamiri njema na imani ya kweli. 6Watu wengine wamepotoka kutoka haya na kugeukia majadiliano yasiyo na maana kwa kuwa, 7wanataka kuwa walimu wa sheria, lakini hawajui mambo yale wanayosema wala hayo wanayoyatumainia kwa uthabiti.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.