1 Timotheo 1:4
1 Timothy 1:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
wala wasitoe muda wao kwa hadithi za kubuniwa na orodha za majina ya vizazi visivyo na mwisho, ambazo huchochea mabishano badala ya mpango wa Mungu utokanao na imani.
1 Timothy 1:4 in English
1 Timothy 1:4 · Berean Standard Bible
or devote themselves to myths and endless genealogies, which promote speculation rather than the stewardship of God’s work, which is by faith.*
Context
2Kwa Timotheo, mwanangu halisi katika imani:
Neema, rehema na amani itokayo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu. 3Kama nilivyokusihi wakati nilipokwenda Makedonia, endelea kubaki Efeso, ili kwamba upate kuwaagiza watu wasiendelee kufundisha mafundisho ya uongo 4wala wasitoe muda wao kwa hadithi za kubuniwa na orodha za majina ya vizazi visivyo na mwisho, ambazo huchochea mabishano badala ya mpango wa Mungu utokanao na imani. 5Kusudi la maagizo haya ni upendo utokao katika moyo safi, dhamiri njema na imani ya kweli. 6Watu wengine wamepotoka kutoka haya na kugeukia majadiliano yasiyo na maana kwa kuwa,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.