1 Samweli 30:4
1 Samuel 30:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hivyo Daudi na watu wake wakapiga yowe mpaka wakaishiwa na nguvu za kulia.
1 Samuel 30:4 in English
1 Samuel 30:4 · Berean Standard Bible
So David and the troops with him lifted up their voices and wept until they had no strength left to weep.
Context
2nao wakawa wamewachukua mateka wanawake pamoja na wote waliokuwamo humo, vijana na wazee. Hawakuua yeyote, bali waliwachukua wakaenda zao. 3Daudi na watu wake walipofika Siklagi, wakakuta mji umeangamizwa kwa moto na wake zao pamoja na wana wao na binti zao wamechukuliwa mateka. 4Hivyo Daudi na watu wake wakapiga yowe mpaka wakaishiwa na nguvu za kulia. 5Wake wawili wa Daudi walikuwa wametekwa: yaani Ahinoamu wa Yezreeli, na Abigaili, mjane wa Nabali wa Karmeli. 6Daudi alihuzunika sana kwa sababu watu walikuwa wakisemezana juu ya kumpiga kwa mawe. Kila mmoja alikuwa na uchungu rohoni kwa sababu ya wanawe na binti zake. Lakini Daudi akajitia nguvu katika Bwana, Mungu wake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.