Native Bible

1 Samuel 30:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Daudi akarudisha kila kitu Waamaleki walikuwa wamechukua, pamoja na wake zake wawili.

1 Samuel 30:18 in English

1 Samuel 30:18 · Berean Standard Bible

So David recovered everything the Amalekites had taken, including his two wives.

Context

16Akamwongoza Daudi mpaka mahali walipokuwa, nao walikuwa wametawanyika eneo lote, wakila, wakinywa na wakifanya karamu kwa sababu ya nyara nyingi walizochukua kutoka nchi ya Wafilisti na kutoka Yuda. 17Daudi akapigana nao kuanzia machweo ya jua hadi kesho yake jioni, na hakuna yeyote miongoni mwao aliyetoroka, isipokuwa vijana wanaume 400 waliopanda ngamia na kutoroka. 18Daudi akarudisha kila kitu Waamaleki walikuwa wamechukua, pamoja na wake zake wawili. 19Hakuna chochote kilichopotea: kijana au mzee, mvulana au msichana, nyara au kitu kingine chochote walichokuwa wamechukua. Daudi akarudisha kila kitu. 20Akachukua makundi yote ya kondoo, mbuzi na ngʼombe, nao watu wake wakawaswaga wanyama hao mbele ya wanyama wengine wa kufugwa, wakisema, “Hizi ni nyara za Daudi.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.