1 Samweli 3:9
1 Samuel 3:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hivyo Eli akamwambia Samweli, “Nenda ukalale, na kama akikuita, sema, ‘Nena Bwana, kwa kuwa mtumishi wako anasikiliza.’ ” Hivyo Samweli akaenda na kulala mahali pake.
1 Samuel 3:9 in English
1 Samuel 3:9 · Berean Standard Bible
“Go and lie down,” he said to Samuel, “and if He calls you, say, ‘Speak, LORD, for Your servant is listening.’” So Samuel went and lay down in his place.
Context
7Wakati huu Samweli alikuwa bado hajamjua Bwana. Neno la Bwana lilikuwa bado halijafunuliwa kwake. 8Bwana akamwita Samweli mara ya tatu, naye Samweli akaamka kwenda kwa Eli na kusema, “Mimi hapa, kwa kuwa umeniita.”
Ndipo Eli akatambua kuwa Bwana alikuwa akimwita kijana. 9Hivyo Eli akamwambia Samweli, “Nenda ukalale, na kama akikuita, sema, ‘Nena Bwana, kwa kuwa mtumishi wako anasikiliza.’ ” Hivyo Samweli akaenda na kulala mahali pake. 10Bwana akaja akasimama hapo, akiita kama mara zile nyingine, “Samweli! Samweli!”
Kisha Samweli akasema, “Nena Bwana, kwa kuwa mtumishi wako anasikiliza.” 11Naye Bwana akamwambia Samweli: “Tazama, nipo karibu kufanya kitu katika Israeli ambacho kitafanya masikio ya kila mmoja atakayesikia yawashe.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.