1 Samweli 3:12
1 Samuel 3:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wakati huo nitatimiza dhidi ya Eli kila kitu nilichonena dhidi ya jamaa yake, kuanzia mwanzo mpaka mwisho.
1 Samuel 3:12 in English
1 Samuel 3:12 · Berean Standard Bible
On that day I will carry out against Eli everything I have spoken about his family, from beginning to end.
Context
10Bwana akaja akasimama hapo, akiita kama mara zile nyingine, “Samweli! Samweli!”
Kisha Samweli akasema, “Nena Bwana, kwa kuwa mtumishi wako anasikiliza.” 11Naye Bwana akamwambia Samweli: “Tazama, nipo karibu kufanya kitu katika Israeli ambacho kitafanya masikio ya kila mmoja atakayesikia yawashe. 12Wakati huo nitatimiza dhidi ya Eli kila kitu nilichonena dhidi ya jamaa yake, kuanzia mwanzo mpaka mwisho. 13Kwa kuwa nilimwambia kwamba ningehukumu jamaa yake milele kwa sababu ya dhambi aliyoijua, wanawe kumkufuru Mungu, naye akashindwa kuwazuia. 14Kwa hiyo, nikaapa kuhusu nyumba ya Eli, ‘Hatia ya nyumba ya Eli kamwe haitaweza kufidiwa kwa dhabihu au sadaka.’ ”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.