Native Bible

1 Samuel 28:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wafilisti wakakusanyika na kupiga kambi yao huko Shunemu, naye Sauli akawakusanya Waisraeli wote na kupiga kambi yao huko Gilboa.

1 Samuel 28:4 in English

1 Samuel 28:4 · Berean Standard Bible

The Philistines came together and camped at Shunem, while Saul gathered all Israel and camped at Gilboa.

Context

2Daudi akasema, “Ndipo wewe mwenyewe utakapojionea jambo ambalo mtumishi wako anaweza kufanya.” Akishi akamjibu Daudi, “Vyema sana, mimi nitakufanya uwe mlinzi wangu daima.” 3Wakati huo Samweli alikuwa amekufa, nao Israeli wote walikuwa wamemwombolezea na kumzika kwenye mji wake mwenyewe huko Rama. Sauli alikuwa amewafukuza waaguzi na wachawi. 4Wafilisti wakakusanyika na kupiga kambi yao huko Shunemu, naye Sauli akawakusanya Waisraeli wote na kupiga kambi yao huko Gilboa. 5Sauli alipoona jeshi la Wafilisti, akaogopa; moyo wake ukajawa na hofu kuu. 6Ndipo Sauli akauliza ushauri kwa Bwana, lakini Bwana hakumjibu kwa ndoto, wala kwa Urimu,* wala kwa njia ya manabii.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.