1 Samweli 27:7
1 Samuel 27:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Daudi akaishi katika nchi ya Wafilisti muda wa mwaka mmoja na miezi minne.
1 Samuel 27:7 in English
1 Samuel 27:7 · Berean Standard Bible
And the time that David lived in Philistine territory amounted to a year and four months.
Context
5Ndipo Daudi akamwambia Akishi, “Kama nimepata kibali machoni pako, unipe sehemu katika mojawapo ya miji katika nchi nikae huko. Kwa nini mtumwa wako akae pamoja nawe katika mji huu wa kifalme?” 6Hivyo siku hiyo Akishi akampa Daudi mji wa Siklagi, nao Siklagi umekuwa mali ya wafalme wa Yuda tangu wakati huo. 7Daudi akaishi katika nchi ya Wafilisti muda wa mwaka mmoja na miezi minne. 8Basi Daudi na watu wake wakapanda na kuwashambulia Wageshuri, Wagirizi na Waamaleki. (Tangu zamani haya mataifa yalikuwa yameishi kwenye eneo lililotanda kuanzia Telemu katika njia iteremkayo Shuri hadi kufikia nchi ya Misri.) 9Kila mara Daudi aliposhambulia eneo, hakubakiza hai mwanaume wala mwanamke, lakini alichukua kondoo na ngʼombe, punda na ngamia, na nguo. Kisha akarudi kwa Akishi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.