1 Samweli 25:12
1 Samuel 25:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Watu wa Daudi wakageuka na kurudi. Walipofika, wakaarifu kila neno.
1 Samuel 25:12 in English
1 Samuel 25:12 · Berean Standard Bible
So David’s men turned around and went back, and they relayed to him all these words.
Context
10Nabali akawajibu watumishi wa Daudi, “Huyu Daudi ni nani? Huyu mwana wa Yese ni nani? Watumishi wengi wanakimbia kutoka kwa bwana zao siku hizi. 11Kwa nini nichukue mkate wangu, maji yangu na nyama niliyochinja kwa ajili ya wakata manyoya wangu, na kuwapa watu ambao hakuna anayejua wanakotoka?” 12Watu wa Daudi wakageuka na kurudi. Walipofika, wakaarifu kila neno. 13Daudi akawaambia watu wake, “Jifungeni panga zenu!” Basi wakajifunga panga zao, naye Daudi akajifunga upanga wake. Watu kama mia nne hivi wakapanda pamoja na Daudi, na watu mia mbili wakabaki na vifaa. 14Mmoja wa watumishi akamwambia Abigaili, mkewe Nabali: “Daudi alituma wajumbe kutoka jangwani kumpa bwana wetu salamu zake, lakini akawavurumishia matukano.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.