1 Samweli 20:28
1 Samuel 20:28 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yonathani akamjibu, “Daudi alinisihi sana nimpe ruhusa aende Bethlehemu.
1 Samuel 20:28 in English
1 Samuel 20:28 · Berean Standard Bible
Jonathan answered, “David urgently requested my permission to go to Bethlehem,
Context
26Sauli hakusema chochote siku ile kwa kuwa alifikiri, “Kuna kitu cha lazima kimetokea kwa Daudi ambacho kimemfanya najisi asihudhurie karamuni, hakika yeye yu najisi.” 27Lakini siku iliyofuata, siku ya pili ya mwezi, kiti cha Daudi kilikuwa wazi tena. Kisha Sauli akamwambia mwanawe Yonathani, “Kwa nini mwana wa Yese hajaja chakulani jana wala leo?” 28Yonathani akamjibu, “Daudi alinisihi sana nimpe ruhusa aende Bethlehemu. 29Alisema, ‘Niruhusu niende, kwa sababu jamaa yetu wana dhabihu mjini, na ndugu yangu ameniagiza niwepo huko. Kama nimepata kibali mbele yako, niruhusu niende kuona ndugu zangu.’ Hii ndiyo sababu hakuja mezani pa mfalme.” 30Hasira ya Sauli ikawaka dhidi ya Yonathani na kumwambia, “Wewe mwana wa mwanamke mkaidi na mwasi! Je, sijui kuwa umekuwa upande wa mwana wa Yese kwa aibu yako mwenyewe na kwa aibu ya mama yako aliyekuzaa?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.