Native Bible

1 Samuel 20:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Yonathani akamwambia, “Njoo, twende shambani.” Basi wakaenda huko pamoja.

1 Samuel 20:11 in English

1 Samuel 20:11 · Berean Standard Bible

“Come,” he replied, “let us go out to the field.” So the two of them went out into the field,

Context

9Yonathani akasema, “La hasha! Kama ningekuwa na kidokezo kidogo kwamba baba yangu amekusudia kukudhuru wewe, je, nisingekuambia?” 10Daudi akamuuliza, “Je, nani atakayeniambia kama baba yako atakujibu kwa ukali?” 11Yonathani akamwambia, “Njoo, twende shambani.” Basi wakaenda huko pamoja. 12Kisha Yonathani akamwambia Daudi, “Ninakuahidi kwa jina la Bwana, Mungu wa Israeli, hakika nitamchunguza baba yangu wakati kama huu kesho kutwa! Kama ameweka utaratibu wa kufaa kukuhusu wewe, je, sitakutumia ujumbe na kukufahamisha? 13Lakini ikiwa baba yangu amenuia kukudhuru, Bwana na anishughulikie kwa ukali, iwapo sitakufahamisha na kukuaga uende salama. Bwana na awe pamoja nawe kama alivyokuwa pamoja na baba yangu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.