1 Samweli 20:10
1 Samuel 20:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Daudi akamuuliza, “Je, nani atakayeniambia kama baba yako atakujibu kwa ukali?”
1 Samuel 20:10 in English
1 Samuel 20:10 · Berean Standard Bible
Then David asked Jonathan, “Who will tell me if your father answers you harshly?”
Context
8Lakini kwa habari yako wewe, mtende wema mtumishi wako, kwa sababu mmeingia kwenye agano pamoja naye mbele za Bwana. Kama nina hatia, basi niue wewe mwenyewe! Kwa nini unikabidhi kwa baba yako?” 9Yonathani akasema, “La hasha! Kama ningekuwa na kidokezo kidogo kwamba baba yangu amekusudia kukudhuru wewe, je, nisingekuambia?” 10Daudi akamuuliza, “Je, nani atakayeniambia kama baba yako atakujibu kwa ukali?” 11Yonathani akamwambia, “Njoo, twende shambani.” Basi wakaenda huko pamoja. 12Kisha Yonathani akamwambia Daudi, “Ninakuahidi kwa jina la Bwana, Mungu wa Israeli, hakika nitamchunguza baba yangu wakati kama huu kesho kutwa! Kama ameweka utaratibu wa kufaa kukuhusu wewe, je, sitakutumia ujumbe na kukufahamisha?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.