1 Samweli 2:26
1 Samuel 2:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Naye kijana Samweli akaendelea kukua katika kimo, akimpendeza Bwana na wanadamu.
1 Samuel 2:26 in English
1 Samuel 2:26 · Berean Standard Bible
And the boy Samuel continued to grow in stature and in favor with the LORD and with man.
Context
24Sivyo, wanangu, hii si habari nzuri ambayo ninasikia ikienea miongoni mwa watu wa Bwana. 25Kama mtu akifanya dhambi dhidi ya mtu mwenzake, mtu mwingine aweza kumwombea kwa Mungu, lakini kama mtu akimfanyia Mungu dhambi, ni nani atakayemwombea?” Hata hivyo wanawe hawakusikia maonyo ya baba yao, kwa sababu Bwana alitaka kuwaua. 26Naye kijana Samweli akaendelea kukua katika kimo, akimpendeza Bwana na wanadamu. 27Basi mtu wa Mungu akaja kwa Eli na kumwambia, “Hivi ndivyo asemavyo Bwana: ‘Je, sikujifunua waziwazi kwa nyumba ya baba yako wakati walikuwa huko Misri chini ya Farao? 28Nilimchagua baba yako kati ya makabila yote ya Israeli kuwa kuhani wangu, kukwea kwenye madhabahu yangu, kufukiza uvumba na kuvaa kisibau mbele yangu. Pia niliwapa nyumba ya baba yako sadaka zote zilizotolewa kwa moto na Waisraeli.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.