1 Samweli 10:24
1 Samuel 10:24 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Samweli akawaambia watu wote, “Je, mnamwona mtu ambaye Bwana amemchagua? Hayupo aliye kama yeye miongoni mwa watu wote.” Ndipo watu wakapiga kelele, wakasema, “Mfalme na aishi maisha marefu.”
1 Samuel 10:24 in English
1 Samuel 10:24 · Berean Standard Bible
Samuel said to all the people, “Do you see the one the LORD has chosen? There is no one like him among all the people.” And all the people shouted, “Long live the king!”
Context
22Wakazidi kuuliza kwa Bwana, “Je, huyo mtu amekwisha kufika hapa?”
Naye Bwana akasema, “Ndiyo, amejificha katikati ya mizigo.” 23Wakakimbia na kumleta kutoka huko, naye aliposimama katikati ya watu, alikuwa mrefu kuliko watu wengine wote. 24Samweli akawaambia watu wote, “Je, mnamwona mtu ambaye Bwana amemchagua? Hayupo aliye kama yeye miongoni mwa watu wote.”
Ndipo watu wakapiga kelele, wakasema, “Mfalme na aishi maisha marefu.” 25Samweli akawaeleza watu madaraka ya ufalme. Akayaandika kwenye kitabu na kuweka mbele za Bwana. Kisha Samweli akawaruhusu watu, kila mmoja aende nyumbani kwake. 26Sauli pia akaenda nyumbani kwake huko Gibea, akisindikizwa na watu hodari ambao Mungu alikuwa amegusa mioyo yao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.