Native Bible

1 Peter 2:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kwenu ninyi mnaoamini, jiwe hili ni la thamani. Lakini kwao wasioamini, “Jiwe walilolikataa waashi limekuwa jiwe kuu la pembeni,”

1 Peter 2:7 in English

1 Peter 2:7 · Berean Standard Bible

To you who believe, then, this stone is precious. But to those who do not believe, “The stone the builders rejected has become the cornerstone,”*

Context

5ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mnajengwa kuwa nyumba ya kiroho, ili mpate kuwa ukuhani mtakatifu, mkitoa dhabihu za kiroho zinazokubaliwa na Mungu kwa njia ya Yesu Kristo. 6Kwa maana imeandikwa katika Maandiko: “Tazama, naweka katika Sayuni, jiwe la pembeni teule lenye thamani, na yeyote atakayemwamini hataaibika kamwe.” 7Kwenu ninyi mnaoamini, jiwe hili ni la thamani. Lakini kwao wasioamini, “Jiwe walilolikataa waashi limekuwa jiwe kuu la pembeni,” 8tena, “Jiwe lenye kuwafanya watu wajikwae, na mwamba wa kuwaangusha.” Wanajikwaa kwa sababu hawakulitii lile neno, kama walivyowekewa tangu zamani. 9Lakini ninyi ni taifa teule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu walio milki ya Mungu, mlioitwa ili kutangaza sifa zake yeye aliyewaita kutoka gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.