Native Bible

1 Kings 9:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Bwana akamtokea mara ya pili, kama alivyokuwa amemtokea huko Gibeoni.

1 Kings 9:2 in English

1 Kings 9:2 · Berean Standard Bible

the LORD appeared to him a second time, as He had appeared to him at Gibeon.

Context

1Solomoni alipomaliza kujenga Hekalu la Bwana na jumba la kifalme, alipokwisha kufanya yote aliyotaka kufanya, 2Bwana akamtokea mara ya pili, kama alivyokuwa amemtokea huko Gibeoni. 3Bwana akamwambia: “Nimesikia dua na maombi uliyofanya mbele zangu, nimeliweka wakfu Hekalu hili ambalo umelijenga, kwa kuweka Jina langu humo milele. Macho yangu na moyo wangu utakuwa humo siku zote. 4“Kukuhusu wewe, kama ukienenda kwa unyofu wa moyo na uadilifu, kama baba yako Daudi alivyofanya na kutenda yote ninayoyaagiza kwa kutunza maagizo yangu na sheria,

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.