1 Wafalme 7:38
1 Kings 7:38 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kisha akatengeneza masinia kumi ya shaba, kila moja likiwa na ujazo wa bathi arobaini,* yakiwa na kipenyo cha dhiraa nne* kila sinia moja kwa kila kimoja ya vile vitako kumi.
1 Kings 7:38 in English
1 Kings 7:38 · Berean Standard Bible
He also made ten bronze basins, each holding forty baths * and measuring four cubits across, one basin for each of the ten stands.
Context
36Alitia nakshi za makerubi, simba na miti ya mitende juu ya uso wa vishikio na juu ya papi, katika kila nafasi iliyopatikana, pamoja na mataji yaliyosokotwa kuzunguka pande zote. 37Hivi ndivyo Hiramu alivyotengeneza vile vitako kumi. Vyote vilikuwa vya kusubu kwenye kalibu za kufanana kwa vipimo na kwa umbo. 38Kisha akatengeneza masinia kumi ya shaba, kila moja likiwa na ujazo wa bathi arobaini,* yakiwa na kipenyo cha dhiraa nne* kila sinia moja kwa kila kimoja ya vile vitako kumi. 39Aliweka vitako vitano upande wa kusini wa Hekalu na vingine vitano upande wa kaskazini. Akaweka ile bahari upande wa kusini, katika pembe ya kusini ya Hekalu. 40Pia akatengeneza masinia, masepetu na mabakuli ya kunyunyizia.
Kwa hiyo Huramu akakamilisha kazi zote katika Hekalu la Bwana kama vile Mfalme Solomoni alikuwa amemwagiza, yaani:
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.