Native Bible

1 Kings 7:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mfalme Solomoni akatuma watu Tiro kumleta Hiramu,

1 Kings 7:13 in English

1 Kings 7:13 · Berean Standard Bible

Now King Solomon sent to bring Huram * from Tyre.

Context

11Sehemu za juu kulikuwepo na mawe yenye ubora wa hali ya juu, yaliyokatwa kwa vipimo na boriti za mierezi. 12Ule ua mkuu ulizungukwa na ukuta wa safu tatu za mawe yaliyochongwa na safu moja ya boriti za mierezi zilizorembwa, kama ulivyokuwa ua wa ndani wa Hekalu la Bwana na baraza yake. 13Mfalme Solomoni akatuma watu Tiro kumleta Hiramu, 14ambaye mama yake alikuwa mjane kutoka kabila la Naftali na baba yake alikuwa mtu wa Tiro tena fundi wa shaba. Hiramu alikuwa na ustadi wa hali ya juu na mzoefu katika aina zote za kazi ya shaba. Alikuja kwa Mfalme Solomoni na kufanya kazi zake zote alizopangiwa. 15Hiramu akasubu nguzo mbili za shaba, kila moja ikiwa na urefu wa dhiraa kumi na nane,* kila nguzo ikiwa na mzingo wa dhiraa kumi na mbili* kwa mstari.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.