1 Wafalme 6:14
1 Kings 6:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Basi Solomoni akajenga Hekalu na kulikamilisha.
1 Kings 6:14 in English
1 Kings 6:14 · Berean Standard Bible
So Solomon built the temple and finished it.
Context
12“Kwa habari ya Hekalu hili unalojenga, kama ukifuata amri zangu, ukatunza masharti yangu na kushika maagizo yangu yote na kuyatii, kwa kupitia wewe nitatimiza ahadi niliyomwahidi Daudi baba yako. 13Nami nitakaa miongoni mwa Waisraeli, nami sitawaacha watu wangu Israeli.” 14Basi Solomoni akajenga Hekalu na kulikamilisha. 15Akazifunika kuta zake za ndani kwa mbao za mierezi, akizipigilia ukutani kuanzia sakafuni mwa Hekalu hadi kwenye dari na kufunika sakafu ya Hekalu kwa mbao za misunobari. 16Akagawa dhiraa ishirini sehemu ya nyuma ya Hekalu kwa mbao za mierezi kuanzia kwenye sakafu hadi darini ili kufanya sehemu takatifu ya ndani, yaani Patakatifu pa Patakatifu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.