1 Wafalme 3:27
1 Kings 3:27 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kisha mfalme akatoa uamuzi wake: “Mpeni mama wa kwanza mtoto aliye hai. Msimuue; ndiye mama yake.”
1 Kings 3:27 in English
1 Kings 3:27 · Berean Standard Bible
Then the king gave his ruling: “Give the living baby to the first woman. By no means should you kill him; she is his mother.”
Context
25Ndipo mfalme akatoa amri: “Mkate mtoto aliye hai vipande viwili; mpe huyu nusu na mwingine nusu.” 26Mwanamke ambaye mwanawe alikuwa hai akajawa na huruma kwa ajili ya mwanawe na kumwambia mfalme, “Tafadhali, bwana wangu, mpe yeye mtoto aliye hai! Usimuue!”
Lakini yule mwanamke mwingine akasema, “Mkate vipande viwili. Asiwe wangu au wake!” 27Kisha mfalme akatoa uamuzi wake: “Mpeni mama wa kwanza mtoto aliye hai. Msimuue; ndiye mama yake.” 28Wakati Israeli yote iliposikia hukumu aliyotoa mfalme, wakamwogopa mfalme, kwa sababu waliona kuwa alikuwa na hekima kutoka kwa Mungu kwa kutoa haki.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.