1 Wafalme 2:15
1 Kings 2:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Akasema, “Kama unavyojua, ufalme ulikuwa wangu. Israeli wote waliniangalia mimi kama mfalme wao. Lakini mambo yalibadilika, ufalme umekwenda kwa ndugu yangu, kwa maana umemjia kutoka kwa Bwana.
1 Kings 2:15 in English
1 Kings 2:15 · Berean Standard Bible
“You know that the kingship was mine,” he said. “All Israel expected that I should reign, but the kingship has turned to my brother, for it has come to him from the LORD.
Context
13Basi Adoniya, mwana wa Hagithi, akaenda kwa Bathsheba, mama yake Solomoni. Bathsheba akamuuliza, “Je, umekuja kwa amani?”
Akajibu, “Ndiyo, kwa amani.” 14Kisha akaongeza, “Ninalo jambo la kukuambia.”
Akajibu, “Waweza kulisema.” 15Akasema, “Kama unavyojua, ufalme ulikuwa wangu. Israeli wote waliniangalia mimi kama mfalme wao. Lakini mambo yalibadilika, ufalme umekwenda kwa ndugu yangu, kwa maana umemjia kutoka kwa Bwana. 16Sasa ninalo ombi moja ninalokuomba. Usinikatalie.”
Bathsheba akasema, “Waweza kuliomba.” 17Kwa hiyo akaendelea kusema, “Tafadhali mwombe Mfalme Solomoni, anipatie Abishagi, Mshunami, awe mke wangu; hatakukatalia wewe.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.