1 Wafalme 17:22
1 Kings 17:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Bwana akasikia kilio cha Eliya, na roho ya kijana ikamrudia, naye akafufuka.
1 Kings 17:22 in English
1 Kings 17:22 · Berean Standard Bible
And the LORD listened to the voice of Elijah, and the child’s life returned to him, and he lived.
Context
20Kisha akamlilia Bwana, akasema “Ee Bwana Mungu wangu, je, pia umeleta msiba juu ya mjane huyu ninayeishi pamoja naye, kwa kusababisha mwanawe kufa?” 21Kisha akajinyoosha juu ya kijana mara tatu na kumlilia Bwana, akisema, “Ee Bwana Mungu wangu, nakuomba roho ya huyu kijana imrudie!” 22Bwana akasikia kilio cha Eliya, na roho ya kijana ikamrudia, naye akafufuka. 23Eliya akamtwaa kijana na kumbeba kutoka chumbani mwake akamshusha kumpeleka kwenye nyumba. Akampa mama yake na kusema, “Tazama, mwanao yu hai!” 24Ndipo yule mwanamke akamwambia Eliya, “Sasa ninajua kwamba wewe ni mtu wa Mungu, na kwamba neno la Bwana kutoka kinywani mwako ni kweli.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.