1 Wafalme 16:31
1 Kings 16:31 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kama vile haikutosha kuishi kama Yeroboamu mwana wa Nebati, akamwoa Yezebeli binti wa Ethbaali, mfalme wa Wasidoni, naye akaanza kumtumikia Baali na kumwabudu.
1 Kings 16:31 in English
1 Kings 16:31 · Berean Standard Bible
And as if it were not enough for him to walk in the sins of Jeroboam son of Nebat, he even married Jezebel the daughter of Ethbaal king of the Sidonians, and he then proceeded to serve and worship Baal.
Context
29Katika mwaka wa thelathini na nane wa utawala wa Asa mfalme wa Yuda, Ahabu mwana wa Omri akawa mfalme wa Israeli, naye akatawala Israeli akiwa Samaria kwa miaka ishirini na miwili. 30Ahabu mwana wa Omri akafanya maovu zaidi machoni mwa Bwana kuliko yeyote aliyewatangulia. 31Kama vile haikutosha kuishi kama Yeroboamu mwana wa Nebati, akamwoa Yezebeli binti wa Ethbaali, mfalme wa Wasidoni, naye akaanza kumtumikia Baali na kumwabudu. 32Akajenga madhabahu kwa ajili ya Baali katika hekalu la Baali lile alilolijenga huko Samaria. 33Pia Ahabu akatengeneza nguzo ya Ashera na kufanya mengi ili kumkasirisha Bwana, Mungu wa Israeli, kuliko walivyofanya wafalme wote wa Israeli waliomtangulia.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.