1 Wafalme 16:27
1 Kings 16:27 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa matukio mengine ya utawala wa Omri, yale aliyofanya na vitu alivyovifanikisha, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli?
1 Kings 16:27 in English
1 Kings 16:27 · Berean Standard Bible
As for the rest of the acts of Omri, along with his accomplishments and the might he exercised, are they not written in the Book of the Chronicles of the Kings of Israel?
Context
25Lakini Omri akatenda maovu machoni pa Bwana na kutenda dhambi kuliko wote waliomtangulia. 26Akaenenda katika njia zote za Yeroboamu mwana wa Nebati na katika dhambi zake, ambazo alisababisha Israeli kutenda, hivyo basi wakamkasirisha Bwana, Mungu wa Israeli kwa sanamu zao zisizofaa. 27Kwa matukio mengine ya utawala wa Omri, yale aliyofanya na vitu alivyovifanikisha, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli? 28Omri akalala pamoja na baba zake na akazikwa huko Samaria. Ahabu mwanawe akatawala mahali pake. 29Katika mwaka wa thelathini na nane wa utawala wa Asa mfalme wa Yuda, Ahabu mwana wa Omri akawa mfalme wa Israeli, naye akatawala Israeli akiwa Samaria kwa miaka ishirini na miwili.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.