1 Wafalme 16:24
1 Kings 16:24 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Alinunua kilima cha Samaria kutoka kwa Shemeri kwa talanta mbili* za fedha na akajenga mji juu ya hicho kilima, akiuita Samaria, kutokana na Shemeri, jina la mmiliki wa kwanza wa kilima hicho.
1 Kings 16:24 in English
1 Kings 16:24 · Berean Standard Bible
He bought the hill of Samaria from Shemer for two talents of silver * and built a city there, calling it Samaria after the name of Shemer, who had owned the hill.
Context
22Lakini wafuasi wa Omri wakajionyesha wenye nguvu kuliko wale wa Tibni mwana wa Ginathi. Hivyo Tibni akafa na Omri akawa mfalme. 23Katika mwaka wa thelathini na moja wa utawala wa Asa mfalme wa Yuda, Omri akawa mfalme wa Israeli, naye akatawala kwa miaka kumi na miwili, sita kati ya hiyo katika Tirsa. 24Alinunua kilima cha Samaria kutoka kwa Shemeri kwa talanta mbili* za fedha na akajenga mji juu ya hicho kilima, akiuita Samaria, kutokana na Shemeri, jina la mmiliki wa kwanza wa kilima hicho. 25Lakini Omri akatenda maovu machoni pa Bwana na kutenda dhambi kuliko wote waliomtangulia. 26Akaenenda katika njia zote za Yeroboamu mwana wa Nebati na katika dhambi zake, ambazo alisababisha Israeli kutenda, hivyo basi wakamkasirisha Bwana, Mungu wa Israeli kwa sanamu zao zisizofaa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.