Native Bible

1 Kings 15:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kulikuwa na vita kati ya Asa na Baasha mfalme wa Israeli siku zote za utawala wao.

1 Kings 15:16 in English

1 Kings 15:16 · Berean Standard Bible

Now there was war between Asa and Baasha king of Israel throughout their days.

Context

14Ijapokuwa hakuondoa mahali pa juu pa kuabudia miungu, moyo wa Asa ulikuwa umejiweka kwa Bwana kikamilifu maisha yake yote. 15Akaleta ndani ya Hekalu la Bwana fedha na dhahabu na vile vyombo ambavyo yeye na baba yake walikuwa wameviweka wakfu. 16Kulikuwa na vita kati ya Asa na Baasha mfalme wa Israeli siku zote za utawala wao. 17Mfalme Baasha wa Israeli akashambulia Yuda na kuweka ngome mji wa Rama ili kumzuia yeyote asitoke wala kuingia nchi ya Mfalme Asa wa Yuda. 18Kisha Asa akachukua fedha yote na dhahabu iliyokuwa imeachwa katika hazina za Hekalu la Bwana na za jumba lake mwenyewe la kifalme. Akawakabidhi maafisa wake na kuwatuma kwa Ben-Hadadi mwana wa Tabrimoni, mwana wa Hezioni, mfalme wa Aramu,* aliyekuwa akitawala Dameski.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.