Native Bible

1 Kings 15:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ijapokuwa hakuondoa mahali pa juu pa kuabudia miungu, moyo wa Asa ulikuwa umejiweka kwa Bwana kikamilifu maisha yake yote.

1 Kings 15:14 in English

1 Kings 15:14 · Berean Standard Bible

The high places were not removed, but Asa’s heart was fully devoted to the LORD all his days.

Context

12Akawafukuza mahanithi wa mahali pa kuabudia miungu kutoka nchi na kuondoa sanamu zote ambazo baba zake walikuwa wametengeneza. 13Hata akamwondoa bibi yake Maaka kwenye wadhifa wake kama mama malkia, kwa sababu alikuwa ametengeneza nguzo ya Ashera ya kuchukiza. Asa akaikata hiyo nguzo na kuiteketeza kwa moto katika Bonde la Kidroni. 14Ijapokuwa hakuondoa mahali pa juu pa kuabudia miungu, moyo wa Asa ulikuwa umejiweka kwa Bwana kikamilifu maisha yake yote. 15Akaleta ndani ya Hekalu la Bwana fedha na dhahabu na vile vyombo ambavyo yeye na baba yake walikuwa wameviweka wakfu. 16Kulikuwa na vita kati ya Asa na Baasha mfalme wa Israeli siku zote za utawala wao.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.