1 Wafalme 15:10
1 Kings 15:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
naye akatawala katika Yerusalemu miaka arobaini na mmoja. Bibi yake aliitwa Maaka binti Abishalomu.
1 Kings 15:10 in English
1 Kings 15:10 · Berean Standard Bible
and he reigned in Jerusalem forty-one years. His grandmother’s * name was Maacah daughter of Abishalom.
Context
8Naye Abiya akalala na baba zake akazikwa katika Mji wa Daudi. Asa mwanawe akawa mfalme baada yake. 9Katika mwaka wa ishirini wa utawala wa Yeroboamu mfalme wa Israeli, Asa akawa mfalme wa Yuda, 10naye akatawala katika Yerusalemu miaka arobaini na mmoja. Bibi yake aliitwa Maaka binti Abishalomu. 11Asa akatenda yaliyo mema machoni mwa Bwana, kama alivyokuwa ametenda Daudi baba yake. 12Akawafukuza mahanithi wa mahali pa kuabudia miungu kutoka nchi na kuondoa sanamu zote ambazo baba zake walikuwa wametengeneza.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.