Native Bible

1 Kings 11:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Solomoni akafuata Ashtorethi mungu mke wa Wasidoni, na Moleki* mungu aliyekuwa chukizo la Waamoni.

1 Kings 11:5 in English

1 Kings 11:5 · Berean Standard Bible

Solomon followed Ashtoreth the goddess of the Sidonians and Milcom * the abomination of the Ammonites.

Context

3Alikuwa na wake 700 mabinti wa uzao wa kifalme, na masuria 300, nao wake zake wakampotosha. 4Kadiri Solomoni alivyozidi kuzeeka, wake zake wakaugeuza moyo wake kuelekea miungu mingine, na moyo wake haukujitolea kikamilifu kwa Bwana Mungu wake, kama ulivyokuwa moyo wa Daudi baba yake. 5Solomoni akafuata Ashtorethi mungu mke wa Wasidoni, na Moleki* mungu aliyekuwa chukizo la Waamoni. 6Kwa hiyo Solomoni akafanya uovu machoni pa Bwana; hakumfuata Bwana kikamilifu kama alivyofanya Daudi baba yake. 7Kwenye kilima mashariki mwa Yerusalemu, Solomoni akajenga mahali pa juu kwa ajili ya Kemoshi chukizo la Wamoabu, na kwa Moleki mungu chukizo la Waamoni.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.